Daniel 7:8 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipokuwa naziangalia hizo pembe, niliona upembe mwingine mdogo ukiota miongoni mwa zile kumi. Ili kuupa nafasi upembe huu zile pembe nyingine tatu zilingolewa pamoja na mizizi yake. Ulikuwa na macho ya binadamu na kinywa kilichotamka maneno ya kujigamba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nilipokuwa nikifikiri kuhusu pembe hizo, mbele yangu kulikuwa na pembe nyingine, ndogo, iliyojitokeza miongoni mwa zile kumi; pembe tatu za mwanzoni ziling’olewa ili kuipa nafasi hiyo ndogo. Pembe hii ilikuwa na macho kama ya mwanadamu, na mdomo ulionena kwa majivuno.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang'olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipokuwa naziangalia hizo pembe, niliona upembe mwingine mdogo ukiota miongoni mwa zile kumi. Ili kuupa nafasi upembe huu zile pembe nyingine tatu ziling'olewa pamoja na mizizi yake. Ulikuwa na macho ya binadamu na kinywa kilichotamka maneno ya kujigamba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Wakati nilipokuwa ninafikiri kuhusu pembe hizo, mbele yangu kulikuwa na pembe nyingine, ambayo ni ndogo, ikajitokeza miongoni mwa zile kumi, pembe tatu za mwanzoni ziling'olewa ili kuipa nafasi hiyo ndogo. Pembe hii ilikuwa na macho kama ya mwanadamu na mdomo ulionena kwa majivuno.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wakati nilipokuwa ninafikiri kuhusu pembe hizo, mbele yangu kulikuwa na pembe nyingine, ambayo ni ndogo, iliyojitokeza miongoni mwa zile kumi; pembe tatu za mwanzoni ziling’olewa ili kuipa nafasi hiyo ndogo. Pembe hii ilikuwa na macho kama ya mwanadamu, na mdomo ulionena kwa majivuno.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipoziangalia hizo pembe, mara nikaona pembe nyingine ndogo iliyotokea katikati yao, nazo hizo pembe za kwanza kwao zikang'olewa tatu mbele yake hiyo, tena pembe hiyo ilikuwa yenye macho kama macho ya mtu na yenye kinywa kilichosema makuu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipokuwa ninaziangalia hizo pembe, niliona pembe ingine ndogo ikiota katikati ya zile kumi, nayo ikaongoa pembe tatu kati ya hizo za kwanza. Pembe ile ilikuwa na macho ya kimutu na kinywa kilichosema maneno ya kujivuna.