Daniel 7:9 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nikiwa bado naangalia, viti vya enzi viliwekwa hapo, kisha ‘Mzee wa kale na kale’ akaja, akaketi. Alikuwa amevaa vazi jeupe kama theluji; nywele zake zilikuwa kama sufu safi. Kiti chake cha enzi kilikuwa cha miali ya moto na magurudumu ya kiti chake yalikuwa ya moto uwakao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nilipoendelea kutazama, “viti vya utawala vikawekwa, naye Mzee wa Siku akaketi. Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji; nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu. Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka miali ya moto, nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nikiwa bado naangalia, viti vya enzi viliwekwa hapo, kisha ‘Mzee wa kale na kale’ akaja, akaketi. Alikuwa amevaa vazi jeupe kama theluji; nywele zake zilikuwa kama sufu safi. Kiti chake cha enzi kilikuwa cha miali ya moto na magurudumu ya kiti chake yalikuwa ya moto uwakao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nilipokuwa ninaendelea kutazama, “viti vya enzi vikawekwa, naye Mzee wa Siku akaketi. Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu. Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka kwa miali ya moto, nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nilipoendelea kutazama, “viti vya enzi vikawekwa, naye Mzee wa Siku akaketi. Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji; nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu. Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka kwa miali ya moto, nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipokuwa nikimtazama, vikaletwa viti vya kifalme; kisha mtu mwenye siku nyingi akaja kukaa, alikuwa amevaa nguo nyeupe zing'aazo kama chokaa juani, nazo nywele za kichwani pake zilikuwa kama manyoya ya kondoo yaliyotakata sana, kiti chake cha kifalme kilikuwa cha miali ya moto, nayo magurudumu ya kiti chake yalikuwa ya moto uwakao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipokuwa nikiendelea kuangalia, nikaona viti vya kifalme viliwekwa hapo, kisha Muzee mumoja wa zamani sana akakuja, akaikaa. Alikuwa amevaa nguo nyeupe kama teluji; nywele zake zilikuwa kama sufu safi. Kiti chake cha kifalme kilikuwa ndimi za moto, na magurudumu ya kiti kile yalikuwa moto unaowaka.