Daniel 8:10 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Upembe huo ulikua sana kufikia viumbe vya mbinguni; ukaziangusha chini baadhi ya nyota na kuzikanyagakanyaga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pembe hiyo ikaendelea kukua hadi kufikia jeshi la mbinguni, nayo ikalitupa baadhi ya nyota za jeshi la angani chini duniani, na kuzikanyaga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Upembe huo ulikua sana kufikia viumbe vya mbinguni; ukaziangusha chini baadhi ya nyota na kuzikanyagakanyaga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pembe hiyo ikaendelea kukua hadi kufikia jeshi la mbinguni, nayo ikalitupa baadhi ya jeshi la vitu vya angani hapa chini duniani na kukanyaga juu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pembe hiyo ikaendelea kukua hadi kufikia jeshi la mbinguni, nayo ikalitupa baadhi ya jeshi la vitu vya angani hapa chini duniani, na kulikanyaga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikakua kufika kwenye kikosi cha mbinguni, vinginevyo vya hicho kikosi ikavibwaga chini nazo nyota mojamoja, ikaziponda kwa kuzikanyagakanyaga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pembe dogo ile ilikomaa sana kufikia viumbe vya mbinguni; ikaangusha chini sehemu ya nyota na kuzikanyagakanyaga.