Daniel 8:11 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Upembe huo ukajikweza juu ya mkuu wa viumbe vya mbinguni. Ukakomesha tambiko za kuteketezwa ambazo mkuu wa viumbe vya mbinguni alitambikiwa kila siku, na kukufuru maskani yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pembe hiyo ikajikweza ili iwe kama Mkuu wa hilo jeshi la Mwenyezi Mungu; ikamwondolea Mwenyezi Mungu dhabihu ya kila siku, napo mahali pake patakatifu pakashushwa chini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Upembe huo ukajikweza juu ya mkuu wa viumbe vya mbinguni. Ukakomesha tambiko za kuteketezwa ambazo mkuu wa viumbe vya mbinguni alitambikiwa kila siku, na kukufuru maskani yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pembe hiyo ikajikweza ili iwe kama Mkuu wa hilo jeshi, ikamwondolea dhabihu ya kila siku, napo mahali pake patakatifu pakashushwa chini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pembe hiyo ikajikweza ili iwe kama Mkuu wa hilo jeshi; ikamwondolea dhabihu ya kila siku, napo mahali pake patakatifu pakashushwa chini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha ikajikuza, imshinde naye Mkuu wa hicho kikosi, kwa hiyo akanyimwa matambiko yake ya kila siku, nalo Kao lake takatifu likaachwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pembe dogo ile ikajitukuza mbele ya mukubwa wa viumbe vya mbinguni. Ikakomesha sadaka za kuteketezwa kwa moto ambazo mukubwa wa viumbe vya mbinguni alivyotambikiwa kila siku, na kuchafua hekalu lake.