Daniel 8:12 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Viumbe vya mbinguni vikatiwa nguvuni mwake pamoja na tambiko za kuteketezwa kila siku, kwa njia ya upotovu. Nao ukweli ukatupwa chini. Upembe huo ukaibwaga chini ibada ya kweli. Ulifanikiwa katika kila jambo ulilofanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu ya uasi, jeshi la watakatifu na dhabihu za kila siku vikatiwa mkononi mwake. Pembe hiyo ikafanikiwa katika kila kitu ilichofanya, nayo kweli ikatupwa chini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Viumbe vya mbinguni vikatiwa nguvuni mwake pamoja na tambiko za kuteketezwa kila siku, kwa njia ya upotovu. Nao ukweli ukatupwa chini. Upembe huo ukaibwaga chini ibada ya kweli. Ulifanikiwa katika kila jambo ulilofanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu ya uasi, jeshi la watakatifu na dhabihu za kila siku vikatiwa mikononi mwake. Ikafanikiwa katika kila kitu ilichofanya, nayo kweli ikatupwa chini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu ya uasi, jeshi la watakatifu na dhabihu za kila siku vikatiwa mikononi mwake. Ikafanikiwa katika kila kitu ilichofanya, nayo kweli ikatupwa chini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nacho hicho kikosi kikatolewa pamoja na yale matambiko kwa kupotolewa; nayo mambo ya kweli ikayatupa chini, hivyo yakaendelea iliyoyafanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Viumbe vya mbinguni vikatiwa chini ya mamlaka yake pamoja na sadaka za kuteketezwa kwa moto za kila siku, kwa ajili ya upotovu. Nao ukweli ukatupwa chini. Pembe dogo ile ikaiangusha chini ibada ya kweli. Ilifanikiwa katika kila jambo iliyofanya.