Daniel 8:13 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kisha, nikamsikia mtakatifu mmoja akizungumza na mwenzake. Huyo mwenzake alimwuliza, ‘Je, matukio yaliyotangazwa na maono haya yataendelea kwa muda gani? Kwa muda gani sadaka za kuteketezwa za kila siku zitabaki zimebatilishwa? Kwa muda gani upotovu wa kuangamiza kila kitu utaendelea, na mahali patakatifu pamoja na viumbe vya mbingu vitaendelea kukanyagwa?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nikamsikia mtakatifu mmoja akizungumza na mtakatifu mwingine, akamwambia, “Je, itachukua muda gani maono haya yatimie: maono kuhusu dhabihu ya kila siku, uasi unaosababisha ukiwa, kutwaliwa kwa mahali patakatifu, na jeshi litakalokanyagwa chini ya nyayo?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kisha, nikamsikia mtakatifu mmoja akizungumza na mwenzake. Huyo mwenzake alimwuliza, ‘Je, matukio yaliyotangazwa na maono haya yataendelea kwa muda gani? Kwa muda gani sadaka za kuteketezwa za kila siku zitabaki zimebatilishwa? Kwa muda gani upotovu wa kuangamiza kila kitu utaendelea, na mahali patakatifu pamoja na viumbe vya mbingu vitaendelea kukanyagwa?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikamsikia mtakatifu mmoja akizungumza na mtakatifu mwingine akamwambia, “Je, itachukua muda gani maono haya yatimie, yaani maono kuhusu dhabihu ya kila siku, uasi unaosababisha ukiwa, kutwaliwa kwa mahali patakatifu na jeshi litakalokanyagwa chini ya nyayo?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikamsikia mtakatifu mmoja akizungumza na mtakatifu mwingine, akamwambia, “Je, itachukua muda gani maono haya yatimie: maono kuhusu dhabihu ya kila siku, uasi unaosababisha ukiwa, kutwaliwa kwa mahali patakatifu, na jeshi litakalokanyagwa chini ya nyayo?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, niliposikia, mtakatifu mmoja akisema: mtakatifu mwingine akamwuliza yuyo huyo aliyesema: Mambo ya hili ono yatakuwa mpaka lini? Hayo ya matambiko ya kila siku na ya mapotovu yanayoangamiza? Nayo yale ya kukitoa Kikao kitakatifu nacho kikosi, vikanyagwekanyagwe?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, nikamusikia mutakatifu mumoja akizungumuza na mwenzake. Huyo mwenzake alimwuliza: Matukio ya mambo yaliyotangazwa katika maono haya yataendelea kwa muda gani? Kwa muda gani sadaka za kuteketezwa za kila siku zitaendelea kuzarauliwa? Kwa muda gani upotovu wa kuangamiza kila kitu utaendelea, na Pahali Patakatifu pamoja na viumbe vya mbingu vitaendelea kukanyagwa?