Daniel 8:15 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Danieli nilipoyaona hayo maono, na nilipokuwa nikijaribu kujua maana yake, ghafla, mmoja kama mwanaadamu akasimama mbele yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi Danieli nilipokuwa ninaangalia maono na kujaribu kuelewa, mbele yangu alisimama mmoja aliyefanana na mwanadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa mimi, naam, mimi Danieli, nilipoyaona maono hayo, nalitafuta kuyafahamu, na tazama, alisimama mbele yangu mmoja mfano wa mwanadamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Danieli nilipoyaona hayo maono, na nilipokuwa nikijaribu kujua maana yake, ghafla, mmoja kama mwanaadamu akasimama mbele yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi Danieli nilipokuwa ninaangalia maono na kujaribu kuelewa, mbele yangu alisimama mmoja anayefanana na mwanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi Danieli nilipokuwa ninaangalia maono na kujaribu kuelewa, mbele yangu alisimama mmoja aliyefanana na mwanadamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi Danieli nilipoiona ndoto hii nikatafuta njia ya kuitambua. Mara nikaona aliyesimama mbele yangu mwenye mwili wa kimtu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa mimi, naam, mimi Danieli, nilipoyaona maono hayo, nalitafuta kuyafahamu, na tazama, alisimama mbele yangu mmoja mfano wa mwanadamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi Danieli nilipoyaona maono hayo, na nilipokuwa nikijaribu kujua maana yake, kwa rafla, nikaona kiumbe kimoja chenye kufanana mwanadamu kikisimama mbele yangu.