Daniel 8:18 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Alipokuwa anazungumza nami, mimi nikashikwa na usingizi mzito huku nimelala kifudifudi. Lakini yeye akanishika na kunisimamisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokuwa akinena nami, nilikuwa katika usingizi mzito, huku nimelala kifudifudi. Ndipo aliponigusa na kunisimamisha wima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi alipokuwa akisema nami, nalishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Alipokuwa anazungumza nami, mimi nikashikwa na usingizi mzito huku nimelala kifudifudi. Lakini yeye akanishika na kunisimamisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipokuwa akinena nami, nilikuwa katika usingizi mzito, huku nimelala kifudifudi. Ndipo aliponigusa na kuniinua nikasimama kwa miguu yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipokuwa akinena nami, nilikuwa katika usingizi mzito, huku nimelala kifudifudi. Ndipo aliponigusa na kunisimamisha wima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliposema nami, nikashikwa na usingizi kabisa, nao uso wangu ukaelekea chini, akanigusa, akanisimamisha tena hapo, nilipokuwa nimesimama,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi alipokuwa akisema nami, nalishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipokuwa anazungumuza nami, mimi nikashikwa na usingizi muzito nikiwa nimelala uso mpaka chini. Lakini yeye akanishika na kunisimamisha.