Daniel 8:22 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ile pembe iliyovunjika na badala yake zikaota pembe nne, ina maana kwamba ufalme huo mmoja utagawanyika kuwa falme nne, lakini falme hizo hazitakuwa na nguvu kama ule ufalme wa kwanza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zile pembe nne zilizoota badala ya ile pembe iliyovunjika zinawakilisha falme nne ambazo zitatokea kutoka taifa lake, lakini hakuna hata mmoja utakaokuwa na nguvu kama ile pembe iliyovunjika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ile pembe iliyovunjika na badala yake zikaota pembe nne, ina maana kwamba ufalme huo mmoja utagawanyika kuwa falme nne, lakini falme hizo hazitakuwa na nguvu kama ule ufalme wa kwanza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zile pembe nne zilizoota badala ya ile pembe iliyovunjika zinawakilisha falme nne ambazo zitatokea kutoka katika taifa lake lakini hakuna hata mmoja utakaokuwa na nguvu kama ule uliovunjika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zile pembe nne zilizoota badala ya ile pembe iliyovunjika zinawakilisha falme nne ambazo zitatokea kutoka taifa lake, lakini hakuna hata mmoja utakaokuwa na nguvu kama ule uliovunjika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena ikivunjika, mahali pake zikitoka nyingine nne, ni kwamba: Nchi za kifalme nne zitatoka katika taifa lake, lakini hazitakuwa na nguvu yake yeye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ile pembe iliyovunjika na pahali pake kukaota pembe ine, ina maana kwamba ufalme huo mumoja utagawanyika kuwa falme ine, lakini falme hizo hazitakuwa na nguvu kama ule ufalme wa kwanza.