Daniel 8:25 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa ujanja wake, atafanikiwa katika mipango yake ya hila, naye atajikweza. Atawaangamiza watu wengi bila taarifa, na atataka kupigana na Mkuu wa wakuu, lakini ataangamizwa pasipo kutumia nguvu za kibinadamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atasababisha udanganyifu ustawi, naye atajihesabu mwenyewe kuwa bora kuliko wote. Wakati watajisikia kuwa salama, atawaangamiza wengi, na kushindana na Mkuu wa wakuu. Lakini ataangamizwa, isipokuwa si kwa uwezo wa mwanadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa ujanja wake, atafanikiwa katika mipango yake ya hila, naye atajikweza. Atawaangamiza watu wengi bila taarifa, na atataka kupigana na Mkuu wa wakuu, lakini ataangamizwa pasipo kutumia nguvu za kibinadamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atasababisha udanganyifu ustawi, naye atajihesabu mwenyewe kuwa bora. Wakati wajisikiapo kuwa wako salama, atawaangamiza wengi na kushindana na Mkuu wa wakuu. Lakini ataangamizwa, isipokuwa si kwa uwezo wa mwanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atasababisha udanganyifu ustawi, naye atajihesabu mwenyewe kuwa bora. Wakati wajisikiapo kuwa wako salama, atawaangamiza wengi, na kushindana na Mkuu wa wakuu. Lakini ataangamizwa, isipokuwa si kwa uwezo wa mwanadamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa werevu wake atayaendesha madanganyo yaliyomo mkononi mwake, atajikuza moyoni mwake, aangamize wengi kwa kuwajia kwa upole. Lakini atakaposimama, ampingie naye aliye Mkuu wa wakuu, ndipo, atakapovunjwa pasipo kukamatwa kwa mikono
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa werevu wake, atafanikiwa katika mipango yake ya udanganyifu, naye atajitukuza. Atawaangamiza watu wengi sana, na atataka kupigana na Mukubwa wa wakubwa, lakini ataangamizwa pasipo kutumia nguvu za kimutu.