Daniel 8:27 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Danieli, nikazimia na kuugua kwa muda. Nilipopona, nikaendelea na shughuli za mfalme. Lakini yale maono yalinistaajabisha, nami sikuweza kuyaelewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi Danieli nilikuwa nimechoka sana, na nikalala nikiwa mgonjwa kwa siku kadhaa. Ndipo nikaamka, nikaendelea na shughuli za mfalme. Nilifadhaishwa na maono hayo; sikuweza kuyaelewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mimi, Danieli, nikazimia, nikaugua siku kadha wa kadha; kisha nikaondoka, nikatenda shughuli za mfalme; nami naliyastajabia yale maono, ila hakuna aliyeyafahamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Danieli, nikazimia na kuugua kwa muda. Nilipopona, nikaendelea na shughuli za mfalme. Lakini yale maono yalinistaajabisha, nami sikuweza kuyaelewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi Danieli, nilikuwa nimechoka sana na nikalala nikiwa mgonjwa kwa siku kadhaa. Ndipo nikaamka nikaenda kwenye shughuli za mfalme. Nilifadhaishwa na maono, nami sikuweza kuyaelewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi Danieli nilikuwa nimechoka sana, na nikalala nikiwa mgonjwa kwa siku kadhaa. Ndipo nikaamka, nikaenda kwenye shughuli za mfalme. Nilifadhaishwa na maono hayo, nami sikuweza kuyaelewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mimi Danieli nikazimia, nikawa mgonjwa siku hizo; kisha nikaondoka kitandani, nikafanya kazi ya kumtumikia mfalame. Lakini nikahangaika sana kwa ajili yao hayo, niliyoyaona, lakini hakuwako aliyenitambua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mimi, Danieli, nikazimia, nikaugua siku kadha wa kadha; kisha nikaondoka, nikatenda shughuli za mfalme; nami naliyastajabia yale maono, ila hakuna aliyeyafaham
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi Danieli, nikazimia na kuugua kwa muda. Nilipopona, nikaendelea na shuguli za mufalme. Lakini yale maono yalishangaza, nami sikuweza kuyaelewa.

Recommended Reading