Daniel 8:3 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipoinua macho yangu, niliona kondoo dume amesimama kando ya mto huo. Kondoo huyo alikuwa na pembe mbili ndefu, lakini moja ilikuwa ndefu zaidi, nayo ilitokea baada ya ile nyingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikatazama juu, na hapo mbele yangu kulikuwa na kondoo dume mwenye pembe mbili, akiwa amesimama kando ya mto, nazo pembe zake zilikuwa ndefu. Pembe moja ilikuwa ndefu kuliko hiyo nyingine, lakini iliendelea kukua baadaye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipoinua macho yangu, niliona kondoo dume amesimama kando ya mto huo. Kondoo huyo alikuwa na pembe mbili ndefu, lakini moja ilikuwa ndefu zaidi, nayo ilitokea baada ya ile nyingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikatazama juu, hapo mbele yangu kulikuwa na kondoo dume mwenye pembe mbili, akiwa amesimama kando ya mto, pembe zake zilikuwa ndefu. Pembe moja ilikuwa ndefu kuliko hiyo nyingine lakini iliendelea kukua baadaye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikatazama juu, na hapo mbele yangu kulikuwa na kondoo dume mwenye pembe mbili, akiwa amesimama kando ya mto, nazo pembe zake zilikuwa ndefu. Pembe moja ilikuwa ndefu kuliko hiyo nyingine, lakini iliendelea kukua baadaye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipoyainua macho yangu, nitazame, mara nikaona dume moja la kondoo aliyesimama hapo penye mto, naye alikuwa na pembe mbili, nazo hizo pembe zilikuwa ndefu, tena moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, nayo hiyo ndefu ndiyo iliyotokea mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipoinua macho yangu, niliona kondoo dume amesimama kando ya muto huo. Kondoo huyo alikuwa na pembe mbili ndefu, lakini moja ilikuwa ndefu zaidi, nayo ilitokea nyuma ya ile ingine.