Daniel 8:4 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilimwona huyo kondoo dume akishambulia kuelekea magharibi, kaskazini na kusini. Hakuna mnyama yeyote aliyethubutu kusimama mbele yake, wala kuzikwepa nguvu zake. Alifanya apendavyo na kujikweza mwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikamtazama yule kondoo dume alivyokuwa akishambulia kuelekea magharibi, kaskazini na kusini. Hakuna mnyama yeyote aliyeweza kusimama mbele yake, wala hakuna aliyeweza kuokoa kutoka nguvu zake. Akafanya kama alivyopenda, naye akawa mkuu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikamwona huyo kondoo mume akisukuma upande wa magharibi, na upande wa kaskazini, na upande wa kusini; wala hakuna mnyama ye yote awezaye kusimama mbele yake, wala hakuna mnyama ye yote awezaye kupokonya mkononi mwake; lakini alitenda kama alivyopenda mwenyewe, akajitukuza nafsi yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilimwona huyo kondoo dume akishambulia kuelekea magharibi, kaskazini na kusini. Hakuna mnyama yeyote aliyethubutu kusimama mbele yake, wala kuzikwepa nguvu zake. Alifanya apendavyo na kujikweza mwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikamtazama yule kondoo alivyokuwa akishambulia kuelekea magharibi, kaskazini na kusini. Hakuna mnyama ye yote aliyeweza kusimama dhidi yake, wala hakuna aliyeweza kuokoa kutoka katika nguvu zake. Alifanya kama atakavyo naye akawa mkuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikamtazama yule kondoo dume alivyokuwa akishambulia kuelekea magharibi, kaskazini na kusini. Hakuna mnyama yeyote aliyeweza kusimama dhidi yake, wala hakuna aliyeweza kuokoa kutoka nguvu zake. Alifanya kama atakavyo, naye akawa mkuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikamwona huyo dume la kondoo, alivyorukia upande wa baharini na wa kaskazini na wa kusini, tena hakuwako nyama yeyote aliyeweza kusimama mbele yake, wala hakuwako aliyeweza kuokoa mkononi mwake, akafanya yaliyompendeza kwa kujikuza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikamwona huyo kondoo mume akisukuma upande wa magharibi, na upande wa kaskazini, na upande wa kusini; wala hakuna mnyama ye yote awezaye kusimama mbele yake, wala hakuna mnyama ye yote awezaye kupokonya mkononi mwake; lakini alitenda kama alivyopenda mwenyewe, akajitukuza nafsi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilimwona huyo kondoo dume akishambulia kuelekea upande wa magaribi, kaskazini na kusini. Hakuna nyama yeyote aliyesubutu kusimama mbele yake, wala kuziepuka nguvu zake. Alifanya sawa anavyopenda na kujitukuza mwenyewe.