Daniel 8:7 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilimwona akimsogelea yule kondoo dume. Alikuwa amemkasirikia sana yule kondoo dume, hivyo akamshambulia kwa nguvu na kuzivunja zile pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuweza kustahimili. Alibwagwa chini na kukanyagwakanyagwa, wala hapakuwa na yeyote wa kumwokoa katika nguvu zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikamwona akimshambulia yule kondoo dume kwa hasira nyingi, akampiga yule kondoo dume na kuvunja pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuwa na nguvu za kumzuia yule beberu; huyo beberu akamwangusha yule kondoo dume chini na kumkanyaga, wala hakuna aliyeweza kumwokoa yule kondoo dume kutoka nguvu za huyo beberu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikamwona akimkaribia kondoo mume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo mume, akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo mume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali akamwangusha chini, akamkanyaga-kanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo mume katika mkono wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilimwona akimsogelea yule kondoo dume. Alikuwa amemkasirikia sana yule kondoo dume, hivyo akamshambulia kwa nguvu na kuzivunja zile pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuweza kustahimili. Alibwagwa chini na kukanyagwakanyagwa, wala hapakuwa na yeyote wa kumwokoa katika nguvu zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikamwona akimshambulia yule kondoo dume kwa hasira nyingi, akimpiga yule kondoo dume na kuvunja pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuwa na nguvu za kumzuia yule beberu, hivyo akamwangusha yule kondoo dume chini na kumkanyaga, wala hakuna aliyeweza kumwokoa yule kondoo dume kutoka katika nguvu za huyo beberu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikamwona akimshambulia yule kondoo dume kwa hasira nyingi, akimpiga yule kondoo dume na kuvunja pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuwa na nguvu za kumzuia yule beberu, hivyo akamwangusha yule kondoo dume chini na kumkanyaga, wala hakuna aliyeweza kumwokoa yule kondoo dume kutoka nguvu za huyo beberu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikamwona, alivyomfikia yule dume la kondoo, akamrukia kwa ukali mwenye uchungu, akampiga yule dume la kondoo, akazivunja pembe zake mbili, naye dume la kondoo hakuwa na nguvu ya kusimama mbele yake, kwa hiyo akambwaga chini, akamkanyagakanyaga, tena hakuwako aliyemwokoa yule dume la kondoo mkononi mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikamwona akimkaribia kondoo mume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo mume, akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo mume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali akamwangusha chini, akamkanyaga-kanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo mume katika mkono wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilimwona akimusogelea yule kondoo dume. Alikuwa amemukasirikia sana yule kondoo dume, hivyo akamushambulia kwa nguvu na kuzivunja zile pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuweza kuvumilia. Aliangushwa chini na kukanyagwakanyagwa, wala hakuna yeyote kwa kumwokoa toka katika nguvu zake.