Daniel 9:10 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tulikataa kukusikiliza, ee Bwana, Mungu wetu; hatukuishi kulingana na sheria zako ulizotupa kwa njia ya watumishi wako manabii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hatukumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, wala kuzishika sheria alizotupatia kupitia kwa watumishi wake, manabii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tulikataa kukusikiliza, ee Bwana, Mungu wetu; hatukuishi kulingana na sheria zako ulizotupa kwa njia ya watumishi wako manabii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hatukumtii BWANA Mungu wetu wala kuzishika sheria alizotupa kupitia kwa watumishi wake manabii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hatukumtii bwana Mwenyezi Mungu wetu wala kuzishika sheria alizotupa kupitia kwa watumishi wake manabii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hatukuisikia sauti ya Bwana Mungu wetu, tuyafuate Maonyo yake, aliyotupa mikononi mwa watumishi wake wafumbuaji, tuyaangalie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wala hatukuitii sauti ya BWANA, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tulikataa kukusikiliza, ee Bwana wetu, Mungu wetu; hatukutenda kulingana na sheria zako ulizotupatia kwa njia ya watumishi wako manabii.