Daniel 9:11 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli wote wameiasi sheria yako, wamekuacha wakakataa kukutii. Kwa sababu tumekukosea, tumemwagiwa laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Mose, mtumishi wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Israeli wote wamekosea sheria yako na kugeuka mbali, nao wamekataa kukutii. “Kwa hiyo laana na viapo vya hukumu vilivyoandikwa katika Torati ya Musa, mtumishi wa Mungu, vimemiminwa juu yetu, kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, Israeli wote wameihalifu sheria yako, kwa kugeuka upande, wasiisikilize sauti yako; basi kwa hiyo laana imemwagwa juu yetu, na uapo ule ulioandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu; kwa sababu tumemtenda dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli wote wameiasi sheria yako, wamekuacha wakakataa kukutii. Kwa sababu tumekukosea, tumemwagiwa laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Mose, mtumishi wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Israeli yote imekosea sheria yako na kugeuka mbali, nao wamekataa kukutii. “Kwa hiyo laana na viapo vya hukumu vilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, mtumishi wa Mungu, vimemiminwa juu yetu, kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Israeli yote imekosea sheria yako na kugeuka mbali, nao wamekataa kukutii. “Kwa hiyo laana na viapo vya hukumu vilivyoandikwa katika Torati ya Musa, mtumishi wa Mungu, vimemiminwa juu yetu, kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waisiraeli wote wakapita tu penye Maonyo yako, wakaenda zao pasipo kuisikia sauti yako; kwa sababu hiyo tukamwagiwa kiapizo, kikatupata nacho kiapo kilichoandikwa katika Maonyo ya Mose, mtumwa wake Mungu, kwani tulimkosea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, Israeli wote wameihalifu sheria yako, kwa kugeuka upande, wasiisikilize sauti yako; basi kwa hiyo laana imemwagwa juu yetu, na uapo ule ulioandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu; kwa sababu tumemtenda dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli wote wameiasi sheria yako, wamekuacha wakakataa kukutii. Kwa sababu tumekukosea, tumemwangiwa laana na viapo vilivyoandikwa katika Sheria ya Musa, mutumishi wako.