Daniel 9:12 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Umethibitisha yale uliyosema utatutenda sisi pamoja na watawala wetu kwa kuuadhibu mji wa Yerusalemu vikali zaidi ya mji mwingine wowote duniani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umetimiza maneno uliyosema dhidi yetu na dhidi ya watawala wetu, kwa kuleta maafa makubwa juu yetu. Chini ya mbingu yote kamwe hapajatendeka kitu kama kile kilichotendeka kwa Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuzi wetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Umethibitisha yale uliyosema utatutenda sisi pamoja na watawala wetu kwa kuuadhibu mji wa Yerusalemu vikali zaidi ya mji mwingine wowote duniani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Umetimiza maneno uliyosema dhidi yetu na dhidi ya watawala wetu kwa kuleta maafa makubwa juu yetu. Chini ya mbingu yote kamwe hapajatendeka kitu kama kile kilichotendeka katika Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Umetimiza maneno uliyosema dhidi yetu na dhidi ya watawala wetu, kwa kuleta maafa makubwa juu yetu. Chini ya mbingu yote kamwe hapajatendeka kitu kama kile kilichotendeka kwa Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akayatimiza maneno yake, aliyoyasema ya kututisha sisi na waamuzi wetu waliotuamua ya kwamba: Atatuletea kibaya kikubwa kisichofanyika po pote chini ya mbingu, kama kitakavyofanyika Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuzi wetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umetimiza yale uliyosema utatutendea sisi pamoja na watawala wetu kwa kuuazibu Yerusalema vikali zaidi ya muji mwingine wowote katika dunia.