Daniel 9:13 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Umetuadhibu kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, lakini mpaka sasa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, hatukuomba msamaha wako kwa kuziacha dhambi zetu na kutafakari uaminifu wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama vile ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, misiba hii yote imekuja juu yetu, lakini hatujaomba fadhili za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kwa kuacha kutenda dhambi na kuisikiliza kweli yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, mabaya haya yote yametupata lakini hata hivyo hatukumwomba Bwana, Mungu wetu, atupe fadhili zake, ili tugeuke na kuyaacha maovu yetu, na kuitambua kweli yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Umetuadhibu kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, lakini mpaka sasa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, hatukuomba msamaha wako kwa kuziacha dhambi zetu na kutafakari uaminifu wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, misiba hii yote imekuja juu yetu, lakini hatujaomba fadhili kwa BWANA Mungu wetu kwa kugeuka kutoka katika dhambi zetu na kuwa wasikivu katika kweli yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, misiba hii yote imekuja juu yetu, lakini hatujaomba fadhili kwa bwana Mwenyezi Mungu wetu kwa kugeuka kutoka dhambi zetu na kuwa wasikivu katika kweli yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vikawa, kama vilivyoandikwa katika Maonyo ya Mose; hicho kibaya chote kikatujia, lakini sisi hatukujipendekeza usoni pa Bwana Mungu wetu tukiyaacha maovu, tuliyoyafanya, tujipatie kwako utambuzi wa kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, mabaya haya yote yametupata lakini hata hivyo hatukumwomba BWANA, Mungu wetu, atupe fadhili zake, ili tugeuke na kuyaacha maovu yetu, na kuitambua kweli yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umetuazibu kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Musa, lakini mpaka sasa, ee Yawe, Mungu wetu, hatukuomba musamaha wako kwa kuziacha zambi zetu na kutambua uaminifu wako.