Daniel 9:14 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ulikuwa tayari kutuadhibu, na ukafanya hivyo, kwa kuwa daima unafanya yaliyo ya haki, nasi hatukukusikiliza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu hakusita kuleta maafa juu yetu, kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ni mwenye haki katika kila afanyalo; lakini hata hivyo, hatujamtii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Bwana ameyavizia mabaya hayo, akatuletea; maana Bwana, Mungu wetu ni mwenye haki katika kazi zake zote azitendazo; na sisi hatukuitii sauti yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ulikuwa tayari kutuadhibu, na ukafanya hivyo, kwa kuwa daima unafanya yaliyo ya haki, nasi hatukukusikiliza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA hakusita kuleta maafa juu yetu, kwa maana BWANA Mungu wetu ni mwenye haki katika kila afanyalo, lakini hata hivyo hatujamtii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana hakusita kuleta maafa juu yetu, kwa maana bwana Mwenyezi Mungu wetu ni mwenye haki katika kila afanyalo; lakini hata hivyo hatujamtii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Bwana akakiangalia hicho kibaya, akifikishe kwetu, kwani Bwana Mungu wetu ni mwongofu, ayanyoshe matendo yake yote, anayoyatenda. Lakini hatukuisikia sauti yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi BWANA ameyavizia mabaya hayo, akatuletea; maana BWANA, Mungu wetu ni mwenye haki katika kazi zake zote azitendazo; na sisi hatukuitii sauti yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, ee Yawe, Mungu wetu, ulikuwa tayari kutuazibu, na ukafanya hivyo, kwa sababu unafanya mambo yanayokuwa ya haki, nasi hatukukusikiliza.