Daniel 9:15 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Na sasa ee Bwana, Mungu wetu, uliyewatoa watu wako nchini Misri kwa nguvu yako kuu na kulifanya jina lako litukuke mpaka sasa, tunasema kwamba tumetenda dhambi; tumefanya maovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sasa, Ee Bwana Mungu wetu, uliyewatoa watu wako Misri kwa mkono wenye nguvu, na kujifanyia Jina linalodumu hadi leo, tumetenda dhambi, tumefanya mabaya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sasa, Ee Bwana Mungu wetu, uliyewatoa watu wako hawa katika nchi ya Misri kwa mkono hodari, ukajipatia sifa, kama ilivyo leo; tumefanya dhambi, tumetenda maovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Na sasa ee Bwana, Mungu wetu, uliyewatoa watu wako nchini Misri kwa nguvu yako kuu na kulifanya jina lako litukuke mpaka sasa, tunasema kwamba tumetenda dhambi; tumefanya maovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sasa, Ee Bwana Mungu wetu, ambaye uliwatoa watu wako Misri kwa mkono wenye nguvu na ambaye umejifanyia Jina linalodumu mpaka leo, tumetenda dhambi, tumefanya mabaya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sasa, Ee Bwana Mungu wetu, ambaye uliwatoa watu wako Misri kwa mkono wenye nguvu, na ambaye umejifanyia Jina linalodumu mpaka leo, tumetenda dhambi, tumefanya mabaya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Lakini na sasa ndiwe Bwana Mungu wetu! Uliwatoa walio ukoo wako katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu ukajipatia Jina, kama inavyojulika leo; nasi tukakukosea, tukaacha kukucha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sasa, Ee Bwana Mungu wetu, uliyewatoa watu wako hawa katika nchi ya Misri kwa mkono hodari, ukajipatia sifa, kama ilivyo leo; tumefanya dhambi, tumetenda maovu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na sasa ee Bwana, Mungu wetu, uliyewaondoa watu wako katika inchi ya Misri kwa nguvu yako kubwa na kulifanya jina lako litukuzwe mpaka sasa, tunasema kwamba tumetenda zambi; tumefanya maovu.