Daniel 9:16 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ee Bwana, kwa kadiri ya matendo yako ya haki usiukasirikie wala kuughadhibikia mji wako wa Yerusalemu, mlima wako mtakatifu. Watu wote wa nchi za jirani wanaudharau mji wa Yerusalemu na watu wako, kwa sababu ya dhambi zetu na maovu waliyotenda wazee wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Bwana, kwa kadiri ya matendo yako ya haki, ondoa hasira yako na ghadhabu yako kwa Yerusalemu, mji wako, mlima wako mtakatifu. Dhambi zetu na maovu ya baba zetu yameifanya Yerusalemu na watu wako kitu cha kudharauliwa kwa wale wote wanaotuzunguka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ee Bwana, kwa kadiri ya matendo yako ya haki usiukasirikie wala kuughadhibikia mji wako wa Yerusalemu, mlima wako mtakatifu. Watu wote wa nchi za jirani wanaudharau mji wa Yerusalemu na watu wako, kwa sababu ya dhambi zetu na maovu waliyotenda wazee wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee Bwana, wewe kwa kadiri ya matendo yako ya haki, ondoa hasira yako na ghadhabu yako juu ya Yerusalemu, mji wako, mlima wako mtakatifu. Dhambi zetu na maovu ya baba zetu yameifanya Yerusalemu na watu wako kitu cha kudharauliwa kwa wale wote wanaotuzunguka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee Bwana, wewe kwa kadiri ya matendo yako ya haki, ondoa hasira yako na ghadhabu yako juu ya Yerusalemu, mji wako, mlima wako mtakatifu. Dhambi zetu na maovu ya baba zetu yameifanya Yerusalemu na watu wako kitu cha kudharauliwa kwa wale wote wanaotuzunguka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana, kwa ajili ya wongofu wako wote nakuomba: Makali yako yenye moto na yarudi nyuma, yauache mji wako wa Yerusalemu, mlima wako mtakatifu ulimo! Kwani kwa ajili ya makosa yetu na kwa ajili ya manza, baba zetu walizozikora, Yerusalemu pamoja na ukoo wako umegeuka kuwa wa kutukanwa tu kwao wote waliokaa na kutuzunguka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Bwana, kwa kadiri ya matendo yako ya haki usiukasirikie wala kuwa na hasira kwa ajili ya muji wako Yerusalema, mulima wako mutakatifu. Watu wote wa inchi za jirani wanauzarau Yerusalema na watu wako, kwa sababu ya zambi zetu na maovu babu zetu waliyotenda.