Daniel 9:18 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tega sikio, ee Mungu wangu; angalia uone taabu tulizo nazo na jinsi unavyotaabika huo mji uitwao kwa jina lako. Tunakutolea maombi yetu si kwa sababu tumetenda haki, bali kwa sababu wewe una huruma nyingi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Mungu, tega sikio, ukasikie; fumbua macho yako ukaone ukiwa wa mji ule wenye Jina lako. Hatukutolei maombi yetu kwa sababu sisi tuna haki, bali kwa sababu ya rehema zako nyingi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tega sikio, ee Mungu wangu; angalia uone taabu tulizo nazo na jinsi unavyotaabika huo mji uitwao kwa jina lako. Tunakutolea maombi yetu si kwa sababu tumetenda haki, bali kwa sababu wewe una huruma nyingi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee Mungu, tega sikio na ukasikie, fumbua macho yako ukaone ukiwa wa mji ule wenye Jina lako. Hatukutolei maombi yetu kwa sababu sisi tuna haki, bali kwa sababu ya rehema zako nyingi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee Mungu, tega sikio na ukasikie; fumbua macho yako ukaone ukiwa wa mji ule wenye Jina lako. Hatukutolei maombi yetu kwa sababu sisi tuna haki, bali kwa sababu ya rehema zako nyingi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu wangu, litege sikio lako, usikie! Yafumbue macho yako, uyaone mabomoko yetu, nao mji huo ulioitwa kwa Jina lako! Kwani tukiyatoa haya malalamiko yetu usoni pako, si kwa wongofu wetu sisi, ila kwa huruma zako nyingi.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tega sikio, ee Mungu wangu; angalia uone taabu tunazokuwa nazo na jinsi huo muji unaoitwa kwa jina lako unavyotaabika. Tunakutolea maombi yetu si kwa sababu tumetenda haki, lakini kwa sababu wewe una huruma nyingi.