Daniel 9:2 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mimi Danieli nilikuwa nikivisoma kwa makini vitabu vitakatifu, na humo nikaelewa maana ya jambo lile Mwenyezi-Mungu alilomfahamisha nabii Yeremia kuhusu ile miaka sabini, muda ambao utahusika na kuharibiwa kwa Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, mimi Danieli nilielewa kutokana na Maandiko, kulingana na neno la Mwenyezi Mungu lililopewa nabii Yeremia, kwamba ukiwa wa Yerusalemu ungetimizwa kwa miaka sabini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mimi Danieli nilikuwa nikivisoma kwa makini vitabu vitakatifu, na humo nikaelewa maana ya jambo lile Mwenyezi-Mungu alilomfahamisha nabii Yeremia kuhusu ile miaka sabini, muda ambao utahusika na kuharibiwa kwa Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake, mimi Danieli, nilielewa kutokana na Maandiko, kulingana na neno la BWANA alilopewa nabii Yeremia, kwamba ukiwa wa Yerusalemu ungetimizwa kwa miaka sabini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, mimi Danieli nilielewa kutokana na Maandiko, kulingana na neno la bwana alilopewa nabii Yeremia, kwamba ukiwa wa Yerusalemu ungetimizwa kwa miaka sabini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
basi, katika mwaka wa kwanza wa ufalme wake, mimi Danieli niliiangalia hesabu ya miaka katika vitabu, ambayo Neno lake Bwana lilimwambia mfumbuaji Yeremia, ya kuwa miaka 70 itamalizika, Yerusalemu ikikaa kuwa mabomoko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mimi Danieli nilikuwa nikisoma kwa uangalifu vitabu vitakatifu, na humo nikaelewa maana ya jambo lile Yawe alilomufahamisha nabii Yeremia juu ya ile miaka makumi saba, muda ambao utahusika na kuharibiwa kwa Yerusalema.