Daniel 9:20 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, nilipokuwa nikiomba, nikiungama dhambi zangu na dhambi za watu wangu wa Israeli, pamoja na kumsihi Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi, nilipokuwa bado nikinena na kuomba, nikiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na nikifanya maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima wake mtakatifu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za Bwana, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, nilipokuwa nikiomba, nikiungama dhambi zangu na dhambi za watu wangu wa Israeli, pamoja na kumsihi Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi, nilipokuwa bado nikinena na kuomba, nikiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli na nikifanya maombi yangu kwa BWANA Mungu wangu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi, nilipokuwa bado nikinena na kuomba, nikiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na nikifanya maombi yangu kwa bwana Mwenyezi Mungu wangu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipokuwa ninasema bado nikiomba na kuyaungama makosa yangu na makosa yao walio ukoo wangu wa Isiraeli na kuyatoa malalamiko yangu usoni pa Bwana Mungu wangu kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za BWANA, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, nilipokuwa nikiomba, nikiitikia zambi zangu na zambi za watu wangu wa inchi ya Israeli, pamoja na kumusihi Yawe kwa ajili ya mulima wake mutakatifu,