Daniel 9:21 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
yule mtu Gabrieli, ambaye nilikuwa nimemwona katika maono hapo awali, alishuka kwa haraka mpaka mahali nilipokuwa. Ilikuwa wakati wa kutoa sadaka ya jioni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wakati nilipokuwa bado katika maombi, Jibraili, yule mtu niliyekuwa nimemwona katika maono hapo awali, alinijia kwa kasi karibu wakati wa kutoa dhabihu ya jioni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
yule mtu Gabrieli, ambaye nilikuwa nimemwona katika maono hapo awali, alishuka kwa haraka mpaka mahali nilipokuwa. Ilikuwa wakati wa kutoa sadaka ya jioni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakati nilipokuwa bado katika maombi, Gabrieli, yule mtu niliyekuwa nimemwona katika maono hapo awali, alinijia kwa kasi karibia na wakati wa kutoa dhabihu ya jioni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakati nilipokuwa bado katika maombi, Jibraili, yule mtu niliyekuwa nimemwona katika maono hapo awali, alinijia kwa kasi karibu wakati wa kutoa dhabihu ya jioni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nilipokuwa ninasema bado na kuyaomba hayo, mara yule mtume Gaburieli, niliyemwona katika ndoto ya kwanza, akaja akiruka upesi, akanigusa saa ile, walipotolea tambiko la jioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
yule mutu Gabrieli, ambaye nilikuwa nimemwona katika maono hapo mbele, alishuka kwa haraka mpaka pahali nilipokuwa. Ilikuwa wakati wa kutoa sadaka ya magaribi.