Daniel 9:24 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Muda wa miaka saba mara sabini umewekwa kwa ajili ya watu wako na juu ya mji wako mtakatifu ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kusamehe uovu, kuleta haki ya milele, kutia mhuri maono na unabii na kupaka mafuta mahali patakatifu kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Majuma sabini yameamriwa kwa ajili ya watu wako na kwa ajili ya mji wako mtakatifu, ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, kuleta haki ya milele, kutia muhuri maono na unabii, na pia kumpaka mafuta yeye aliye mtakatifu sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Muda wa miaka saba mara sabini umewekwa kwa ajili ya watu wako na juu ya mji wako mtakatifu ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kusamehe uovu, kuleta haki ya milele, kutia mhuri maono na unabii na kupaka mafuta mahali patakatifu kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Majuma sabini yameamuriwa kwa ajili ya watu wako na kwa ajili ya mji wako mtakatifu ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, kuleta haki ya milele, kutia muhuri maono na unabii pia kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Majuma sabini yameamriwa kwa ajili ya watu wako na kwa ajili ya mji wako mtakatifu, ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, kuleta haki ya milele, kutia muhuri maono na unabii, na pia kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Majuma 70 ndiyo, waliyokatiwa walio ukoo wako na wa mji wako mtakatifu ya kuyalipa mapotovu na kuyakomesha makosa na kuzifunika manza, walizozikora, na kuleta wongofu wa kale na kale na kuyatia muhuri maono ya wafumbuaji na kupaeua Patakatifu Penyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muda wa miaka saba mara makumi saba umewekwa kwa ajili ya watu wako na juu ya muji wako mutakatifu kwa kumaliza makosa, kukomesha zambi, kusamehe uovu, kuleta haki ya milele, kutia muhuri juu ya maono na unabii na kupakaa mafuta katika Pahali Patakatifu Sana.