Daniel 9:25 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ujue na kufahamu jambo hili: Tangu wakati itakapotolewa amri ya kujengwa upya mji wa Yerusalemu hadi kuja kwake aliyepakwa mafuta, yule aliye mkuu, ni muda wa majuma saba. Kwa muda wa majuma sitini na mawili, mji wa Yerusalemu utajengwa upya, wenye barabara kuu na mahandaki, lakini wakati huo utakuwa wa taabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ujue na kuelewa hili: Tangu kutolewa kwa amri ya kuutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hadi kuja kwa Mpakwa mafuta, aliye mtawala, kutakuwa na majuma saba, na majuma sitini na mawili. Barabara zitajengwa tena pamoja na mahandaki, lakini katika wakati wa taabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ujue na kufahamu jambo hili: tangu wakati itakapotolewa amri ya kujengwa upya mji wa Yerusalemu hadi kuja kwake aliyepakwa mafuta, yule aliye mkuu, ni muda wa majuma saba. Kwa muda wa majuma sitini na mawili, mji wa Yerusalemu utajengwa upya, wenye barabara kuu na mahandaki, lakini wakati huo utakuwa wa taabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ujue na kuelewa hili: Tangu kutolewa kwa amri ya kuutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu mpaka kuja kwa Mpakwa mafuta, aliye mtawala, kutakuweko majuma saba na majuma sitini na mawili. Barabara zitajengwa tena pamoja na mahandaki, lakini katika wakati wa taabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ujue na kuelewa hili: Tangu kutolewa kwa amri ya kuutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu mpaka kuja kwa Mpakwa mafuta, aliye mtawala, kutakuwako majuma saba na majuma sitini na mawili. Barabara zitajengwa tena pamoja na mahandaki, lakini katika wakati wa taabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ujue na kuvitambua vema: Tangu hapo lilipotoka lile neno la kuujenga Yerusalemu tena, mpaka kutokea kwake mkuu aliyepakwa mafuta ni majuma 7, tena majuma 62 utajengwa tena viwanja na boma, lakini siku zile zitakuwa za kusongwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ujue na kufahamu jambo hili: tangu wakati amri itakapotolewa ya kujengwa upya Yerusalema mpaka kuja kwa yule aliyepakwa mafuta, yule anayekuwa mukubwa, ni muda wa majuma saba. Kwa muda wa majuma makumi saba na mawili, Yerusalema utajengwa upya, wenye barabara kubwa na kuta, lakini wakati huo utakuwa wa taabu.