Daniel 9:26 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya majuma hayo sitini na mawili, yule aliyepakwa mafuta atakatiliwa mbali hatabaki na kitu. Mji na mahali patakatifu kabisa vitaharibiwa na jeshi la mtawala atakayekuja kushambulia. Mwisho wake utafika kama mafuriko, kukiwa na vita na maangamizi kama yalivyopangwa na Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya majuma sitini na mawili, Mpakwa Mafuta atakatiliwa mbali, wala hatabaki na kitu. Watu wa mtawala atakayekuja watauharibu mji pamoja na mahali patakatifu. Mwisho utakuja kama mafuriko: Vita vitaendelea hadi mwisho, nao ukiwa umeamriwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya majuma hayo sitini na mawili, yule aliyepakwa mafuta atakatiliwa mbali hatabaki na kitu. Mji na mahali patakatifu kabisa vitaharibiwa na jeshi la mtawala atakayekuja kushambulia. Mwisho wake utafika kama mafuriko, kukiwa na vita na maangamizi kama yalivyopangwa na Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya majuma sitini na mawili Mpakwa mafuta atakatiliwa mbali wala hatabakia na kitu. Watu wa mtawala atakayekuja watauharibu mji pamoja na mahali patakatifu. Mwisho utakuja kama mafuriko: Vita vitaendelea mpaka mwisho, nao ukiwa umeamriwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya majuma sitini na mawili, Mpakwa Mafuta atakatiliwa mbali, wala hatabaki na kitu. Watu wa mtawala atakayekuja watauharibu mji pamoja na mahali patakatifu. Mwisho utakuja kama mafuriko: Vita vitaendelea mpaka mwisho, nao ukiwa umeamriwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo majuma 62 yatakapokwisha, ndipo, yeye aliyepakwa mafuta atakapoangamizwa, naye atakuwa hanalo kosa lo lote. Kisha watu wa mkuu atakayekuja wataubomoa huo mji napo Patakatifu, nao mwisho wake utakuwa wa kufurikiwa na maji, tena mpaka mwisho yatakuwa mapigano na maangamizo, waliyotakiwa kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha majuma hayo makumi saba na mawili, yule aliyepakwa mafuta atauawa na hatabaki na kitu. Muji na Pahali Patakatifu Sana vitaharibishwa na waaskari wa mutawala atakayekuja kushambulia. Mwisho wake utafika kama mafuriko, kukiwa vita na maangamizi kama yalivyopangwa na Mungu.