Daniel 9:27 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtawala huyo atafanya mapatano imara na watu wengi kwa muda wa miaka saba. Baada ya nusu ya muda huo atakomesha tambiko na sadaka. Mahali pa juu hekaluni patasimamishwa chukizo haribifu, nalo litabaki hapo mpaka yule aliyelisimamisha atakapoangamizwa kama ilivyopangwa na Mungu.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtawala huyo atathibitisha agano na watu wengi kwa juma moja. Katikati ya juma hilo atakomesha dhabihu na sadaka. Mahali pa dhabihu katika Hekalu, atasimamisha chukizo la uharibifu, hadi mwisho ulioamriwa utakapomiminwa juu yake yeye aletaye uharibifu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtawala huyo atafanya mapatano imara na watu wengi kwa muda wa miaka saba. Baada ya nusu ya muda huo atakomesha tambiko na sadaka. Mahali pa juu hekaluni patasimamishwa chukizo haribifu, nalo litabaki hapo mpaka yule aliyelisimamisha atakapoangamizwa kama ilivyopangwa na Mungu.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtawala huyo atathibitisha agano na watu wengi kwa juma moja. Katikati ya juma hilo atakomesha dhabihu na sadaka. Mahali pa dhabihu katika Hekalu atasimamisha chukizo la uharibifu, hadi mwisho ulioamuriwa utakapomiminwa juu yake yeye aletaye uharibifu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtawala huyo atathibitisha agano na watu wengi kwa juma moja. Katikati ya juma hilo atakomesha dhabihu na sadaka. Mahali pa dhabihu katika Hekalu atasimamisha chukizo la uharibifu, hadi mwisho ulioamriwa utakapomiminwa juu yake yeye aletaye uharibifu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye atafanyia wengi agano lenye nguvu la juma 1, kisha hilo juma litakapofika kati, atawakomesha watu, wasitoe wala ng'ombe wala vilaji vya tambiko, napo pembeni pa kutambikia atasimama mwangamizaji atapishaye, mpaka yatimie na kumfurikia yeye mwangamizaji, aliyotakiwa kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutawala huyo atafanya mapatano imara na watu wengi kwa muda wa miaka saba. Kisha nusu ya muda huo atakomesha sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka zingine. Pahali pa juu katika hekalu patasimamishwa chukizo linaloleta uharibifu, nalo litabaki pale mpaka yule aliyemusimamisha atakapoangamizwa kama ilivyopangwa na Mungu.