Daniel 9:4 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilimwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, na kuungama, nikisema: “Ee Bwana, wewe ni Mungu mkuu na wa kuogofya. Wewe ni mwaminifu kwa agano lako na unawafadhili wakupendao na kuzitii amri zako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikamwomba Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, na kutubu: “Ee Bwana, Mungu mkuu na unayetisha, anayeshika agano lake la upendo kwao wanaompenda na kutii maagizo yake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilimwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, na kuungama, nikisema: “Ee Bwana, wewe ni Mungu mkuu na wa kuogofya. Wewe ni mwaminifu kwa agano lako na unawafadhili wakupendao na kuzitii amri zako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikamwomba BWANA Mungu wangu na kutubu: “Ee Bwana, Mungu mkuu na unayetisha, anayeshika Agano lake la upendo kwao wanaompenda na kutii maagizo yake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikamwomba bwana Mwenyezi Mungu wangu na kutubu: “Ee Bwana, Mungu mkuu na unayetisha, anayeshika agano lake la upendo kwao wanaompenda na kutii maagizo yake,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikamwomba Bwana Mungu wangu nikiungana na kusema hivyo: E Bwana, ndiwe Mungu mkuu aogopeshaye, unalishika agano la kuwahurumia wakupendao na kuyashika maagizo yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikamwomba BWANA, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilimwomba Yawe, Mungu wangu, na kuitikia zambi, nikisema: Ee Bwana, wewe ni Mungu mukubwa na wa kuogopesha. Wewe unashika agano lako na kutenda mema kwa wanaokupenda na kuzitii amri zako.