Daniel 9:7 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwako, ee Bwana, kuna uadilifu, lakini sisi daima tumejaa aibu. Jambo hili ni kweli kwetu sote tuishio Yudea, wakazi wa mji wa Yerusalemu na Waisraeli wote ambao umewatawanya katika nchi za mbali na za karibu kwa sababu ya kukosa uaminifu kwako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Bwana, wewe ni mwenye haki, lakini siku hii ya leo tumefunikwa na aibu: watu wa Yuda, na wakaaji wa Yerusalemu, na Waisraeli wote, walio karibu na walio mbali, katika nchi zote ulikotutawanya kwa sababu tulikosa uaminifu kwako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwako, ee Bwana, kuna uadilifu, lakini sisi daima tumejaa aibu. Jambo hili ni kweli kwetu sote tuishio Yudea, wakazi wa mji wa Yerusalemu na Waisraeli wote ambao umewatawanya katika nchi za mbali na za karibu kwa sababu ya kukosa uaminifu kwako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Bwana, wewe ni mwenye haki, lakini siku hii ya leo tumefunikwa na aibu, wanaume wa Yuda na watu wa Yerusalemu nayo Israeli yote, wote walio karibu na walio mbali, katika nchi zote ulikotutawanya kwa sababu ya sisi kukosa uaminifu kwako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Bwana, wewe ni mwenye haki, lakini siku hii ya leo tumefunikwa na aibu: tukiwa wanaume wa Yuda, na watu wa Yerusalemu, na Israeli yote, wote walio karibu na walio mbali, katika nchi zote ulikotutawanya kwa sababu ya kukosa uaminifu kwako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe Bwana u mwenye wongofu, lakini sisi nyuso zinatuiva kwa soni; ndivyo, vinavyojulika leo: sisi waume wa Yuda nao wakaao Yerusalemu nao Waisiraeli wote walioko karibu nao walioko mbali katika nchi zote, ulikowatawanyia kwa ajili ya matendo yao, waliyokutendea,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwako, ee Bwana, kuna haki, lakini sisi tumepata haya siku zote. Jambo hili ni kweli kwetu sisi wote tunaoishi Yudea, wakaaji wa muji Yerusalema na Waisraeli wote ambao umewatawanya katika inchi za mbali na za karibu kwa sababu ya kukosa uaminifu kwako.