Deuteronomy 1:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, na awafanye mzidi kuongezeka mara elfu zaidi ya mlivyo sasa na kuwabariki kama alivyoahidi!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, na awaongeze mara elfu na kuwabariki kama alivyoahidi!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabarikia, kama alivyowaahidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, na awafanye mzidi kuongezeka mara elfu zaidi ya mlivyo sasa na kuwabariki kama alivyoahidi!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye BWANA, Mungu wa baba zenu na awaongeze mara elfu na kuwabariki kama alivyoahidi!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye bwana, Mungu wa baba zenu na awaongeze mara elfu na kuwabariki kama alivyoahidi!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabariki, kama alivyowaahidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, na awafanye mzidi kuongezeka mara elfu zaidi ya mlivyo sasa na kuwabariki kama alivyoahidi!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mungu wa baba zenu na aendelee kuwafanya kuwa wengi zaidi, wao walioko sasa waongezeke mara elfu, kisha na awabariki, kama alivyowaambia ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabarikia, kama alivyowaahidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe, Mungu wa babu zenu, awafanye muzidi kuongezeka mara elfu zaidi ya vile munavyokuwa sasa na kuwabariki kama vile alivyoahidi!