Deuteronomy 1:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyotuamuru, tulianza safari yetu kutoka mlima Horebu, tukapita katika lile jangwa kubwa la kutisha mnalolijua, kwa kufuata njia inayoelekea nchi ya milima ya Waamori. Tulipofika Kadesh-barnea,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha, kama Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, alivyotuamuru, tuliondoka kutoka Horebu na kwenda kuelekea nchi ya vilima ya Waamori, kupitia jangwa lile kubwa lote la kutisha, lile mliloliona, nasi tukafika Kadesh-Barnea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama Bwana, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyotuamuru, tulianza safari yetu kutoka mlima Horebu, tukapita katika lile jangwa kubwa la kutisha mnalolijua, kwa kufuata njia inayoelekea nchi ya milima ya Waamori. Tulipofika Kadesh-barnea,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha, kama BWANA Mungu wetu alivyotuamuru, tuliondoka kutoka Horebu na kwenda kuelekea nchi ya vilima ya Waamori, kupitia jangwa lile kubwa lote la kutisha, lile mliloliona, nasi tukafika Kadesh-Barnea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha, kama bwana Mwenyezi Mungu wetu alivyotuamuru, tuliondoka kutoka Horebu na kwenda kuelekea nchi ya vilima ya Waamori, kupitia jangwa lile kubwa lote la kutisha, lile mliloliona, nasi tukafika Kadesh-Barnea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama BWANA, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi, kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyotuamuru, tulianza safari yetu kutoka mlima Horebu, tukapita katika lile jangwa kubwa la kutisha mnalolijua, kwa kufuata njia inayoelekea nchi ya milima ya Waamori. Tulipofika Kadesh-barnea,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tulipoondoka Horebu tukasafiri katika ile nyika yote inayotisha kwa ukubwa wake, kama mlivyoona; tukaishika njia ya kwenda milimani kwa Waamori, kama Bwana Mungu wetu alivyotuagiza, tukafika mpaka Kadesi-Barnea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama BWANA, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Basi, kama vile Yawe, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukaanza safari yetu kutoka mulima Horebu, tukapita katika lile jangwa kubwa la kutisha munalojua, kwa kufuata njia inayoelekea inchi ya milima ya Waamori. Tulipofika Kadesi-Barnea,