Deuteronomy 1:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliporudi, walituletea baadhi ya matunda ya nchi hiyo na wakatuarifu kwamba nchi hiyo anayotupatia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni nzuri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakachukua baadhi ya matunda ya nchi, wakatuletea na kutuarifu, “Ni nchi nzuri ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, anatupatia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakatwaa baadhi ya matunda ya nchi ile mikononi mwao, wakatuletea huku chini, wakatuletea habari tena, wakasema, Nchi hii anayotupa Bwana, Mungu wetu, ni nchi njema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliporudi, walituletea baadhi ya matunda ya nchi hiyo na wakatuarifu kwamba nchi hiyo anayotupatia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni nzuri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakachukua baadhi ya matunda ya nchi, wakatuletea na kutuarifu, “Ni nchi nzuri ambayo BWANA Mungu wetu anatupa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakachukua baadhi ya matunda ya nchi, wakatuletea na kutuarifu, “Ni nchi nzuri ambayo bwana Mwenyezi Mungu wetu anatupa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakachuma baadhi ya matunda ya nchi ile mikononi mwao, wakatuletea huku chini, wakatuletea habari tena, wakasema, Nchi hii anayotupa BWANA, Mungu wetu, ni nchi njema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliporudi, walituletea baadhi ya matunda ya nchi hiyo na wakatuarifu kwamba nchi hiyo anayotupatia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni nzuri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakachukua kwa mikono yao matunda mengineyo ya nchi hiyo, wakashuka nayo kutuletea sisi, wakatuletea nazo habari za kwamba: Nchi hii, Bwana Mungu wetu anayotaka kutupa, ni nzuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakatwaa baadhi ya matunda ya nchi ile mikononi mwao, wakatuletea huku chini, wakatuletea habari tena, wakasema, Nchi hii anayotupa BWANA, Mungu wetu, ni nchi njema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waliporudi, wakatuletea matunda mamoja ya inchi hiyo na wakatuarifu kwamba inchi hiyo Yawe, Mungu wetu, anayotupatia ni nzuri.