Deuteronomy 1:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kule jangwani ambako mliona jinsi alivyowabeba safari hiyo yote kama vile baba amchukuavyo mwanawe mpaka mkafika hapa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na pia huko jangwani. Huko mliona jinsi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alivyowachukua, kama baba amchukuavyo mwanawe, katika njia yote mliyoiendea hadi mkafika mahali hapa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua Bwana, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafikilia mahali hapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kule jangwani ambako mliona jinsi alivyowabeba safari hiyo yote kama vile baba amchukuavyo mwanawe mpaka mkafika hapa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na pia huko jangwani. Huko mliona jinsi BWANA Mungu wenu alivyowachukua, kama baba amchukuavyo mwanawe, katika njia yote mliyoiendea mpaka mkafika mahali hapa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na pia huko jangwani. Huko mliona jinsi bwana Mwenyezi Mungu wenu alivyowachukua, kama baba amchukuavyo mwanawe, katika njia yote mliyoiendea mpaka mkafika mahali hapa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua BWANA, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafika mahali hapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kule jangwani ambako mliona jinsi alivyowabeba safari hiyo yote kama vile baba amchukuavyo mwanawe mpaka mkafika hapa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nako nyikani mmeona, Bwana Mungu wenu alivyowachukua, kama mtu anavyomchukua mwanawe, katika hizo safari zote, mlizokwenda, mpaka mkifika mahali hapa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua BWANA, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafikilia mahali hapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kule katika jangwa ambako muliona jinsi alivyowabeba safari hiyo yote kama vile baba anavyobeba mwana wake, mpaka mukafika hapa.