Deuteronomy 1:41 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kisha mkanijibu, ‘Sisi tumemtendea dhambi Mwenyezi-Mungu, lakini sasa tutakwenda na kupigana kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyotuamuru’. Hivyo, kila mmoja wenu akajitayarisha kupigana vita; maana mlifikiri kwamba lingekuwa jambo rahisi kuivamia nchi hiyo ya milima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo mkanijibu, “Tumemtenda Mwenyezi Mungu dhambi. Tutaenda kupigana, kama Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, alivyotuamuru.” Hivyo kila mmoja wenu akachukua silaha zake, huku mkifikiri kuwa ni rahisi kukwea katika nchi ya vilima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mkanijibu, mkaniambia, Sisi tumefanya dhambi juu ya Bwana, tutakwea kupigana kwa mfano wa yote tuliyoamriwa na Bwana. Mkajifunga kila mtu silaha zake za vita, mkafanya wepesi kukwea mlimani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kisha mkanijibu, ‘Sisi tumemtendea dhambi Mwenyezi-Mungu, lakini sasa tutakwenda na kupigana kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyotuamuru’. Hivyo, kila mmoja wenu akajitayarisha kupigana vita; maana mlifikiri kwamba lingekuwa jambo rahisi kuivamia nchi hiyo ya milima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo mkanijibu, “Tumemtenda BWANA dhambi. Tutakwenda kupigana, kama BWANA Mungu wetu alivyotuamuru.” Hivyo kila mmoja wenu akachukua silaha zake, huku mkifikiri kuwa ni rahisi kukwea katika nchi ya vilima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo mkanijibu, “Tumemtenda bwana dhambi. Tutakwenda kupigana, kama bwana Mwenyezi Mungu wetu alivyotuamuru.” Hivyo kila mmoja wenu akachukua silaha zake, huku mkifikiri kuwa ni rahisi kukwea katika nchi ya vilima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo mkanijibu, mkaniambia, Sisi tumefanya dhambi juu ya BWANA, tutakwea kupigana kwa mfano wa yote tuliyoamriwa na BWANA. Mkajihami kila mtu na silaha zake za vita, mkafanya wepesi kukwea mlimani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kisha mkanijibu, ‘Sisi tumemtendea dhambi Mwenyezi-Mungu, lakini sasa tutakwenda na kupigana kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyotuamuru’. Hivyo, kila mmoja wenu akajitayarisha kupigana vita; maana mlifikiri kwamba lingekuwa jambo rahisi kuivamia nchi hiyo ya milima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mlipojibu na kuniambia: Tumemkosea Bwana. Sisi na tupande, tupige vita na kuyafanya yote, Bwana Mungu wetu aliyotuagiza. Lakini hapo mlipojifunga mata yenu ya kupigia vita kwa kuwaza, ya kama ni kazi nyepesi kupanda huko milimani,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mkanijibu, mkaniambia, Sisi tumefanya dhambi juu ya BWANA, tutakwea kupigana kwa mfano wa yote tuliyoamriwa na BWANA. Mkajifunga kila mtu silaha zake za vita, mkafanya wepesi kukwea mlimani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kisha mukanijibu: ‘Sisi tumemutendea Yawe zambi, lakini sasa tutakwenda na kupigana kama vile Yawe, Mungu wetu alivyotuamuru’. Hivyo, kila mumoja wenu akajitayarisha kupigana vita, maana mulifikiri kwamba lingekuwa jambo jepesi kuishambulia inchi hiyo ya milima.