Deuteronomy 1:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
sasa vunjeni kambi yenu mwendelee na safari. Nendeni kwenye nchi ya milima ya Waamori na maeneo ya nchi jirani katika Araba, kwenye milima na mabonde, huko Negebu na sehemu za pwani; naam, nendeni mpaka nchi ya Kanaani, na nchi ya Lebanoni, hadi kwenye ule mto mkubwa wa Eufrate.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vunjeni kambi, msonge mbele kuelekea nchi ya vilima ya Waamori; nendeni kwa watu wote ambao ni majirani wa Araba, katika milima, Shefela, katika Negebu na kandokando ya pwani, hadi nchi ya Wakanaani na hadi Lebanoni, na kufika mto mkubwa Frati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima-vilima, na huko Shefela, na Negebu, na pwani-pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
sasa vunjeni kambi yenu mwendelee na safari. Nendeni kwenye nchi ya milima ya Waamori na maeneo ya nchi jirani katika Araba, kwenye milima na mabonde, huko Negebu na sehemu za pwani; naam, nendeni mpaka nchi ya Kanaani, na nchi ya Lebanoni, hadi kwenye ule mto mkubwa wa Eufrate.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vunjeni kambi, msonge mbele kuelekea katika nchi ya vilima ya Waamori; nendeni kwa watu wote ambao ni majirani wa Araba, katika milima, upande wa magharibi chini ya vilima, katika Negebu na kandokando ya pwani, mpaka nchi ya Wakanaani hadi Lebanoni, na kufika mto mkubwa Eufrati.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vunjeni kambi, msonge mbele kuelekea nchi ya vilima ya Waamori; nendeni kwa watu wote ambao ni majirani wa Araba, katika milima, upande wa magharibi chini ya vilima, katika Negebu na kandokando ya pwani, mpaka nchi ya Wakanaani hadi Lebanoni, na kufika mto mkubwa Frati.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima vilima, na huko Shefela, na Negebu, na pwani pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
sasa vunjeni kambi yenu mwendelee na safari. Nendeni kwenye nchi ya milima ya Waamori na maeneo ya nchi jirani katika Araba, kwenye milima na mabonde, huko Negebu na sehemu za pwani; naam, nendeni mpaka nchi ya Kanaani, na nchi ya Lebanoni, hadi kwenye ule mto mkubwa wa Eufrate.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo ondokeni huku na kujielekeza kwenda milimani kwa Waamori nako kwao wote wanaokaa karibu yao nyikani na milimani na mabondeni na kusini na pwani kwenye bahari, mfike katika nchi ya Kanaani hata Libanoni mpaka ule mto mkubwa, lile jito la Furati.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima-vilima, na huko Shefela, na Negebu, na pwani-pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa muvunje kambi yenu muendelee na safari. Muende kwenye inchi ya milima ya Waamori na maeneo ya inchi jirani katika Araba, kwenye milima na mabonde, huko Negebu na sehemu za pembeni ya bahari. Muende mpaka inchi ya Kanana, na inchi ya Lebanoni, mpaka kwenye ule muto mukubwa Furati.