Deuteronomy 10:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ndiye Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana. Yeye ni Mungu mkuu na mwenye nguvu, na wa kuogofya; hapendelei wala hapokei rushwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ndiye Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana. Yeye ni Mungu mkuu na mwenye nguvu, na wa kuogofya; hapendelei wala hapokei rushwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa BWANA Mungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea watu, wala kukubali rushwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ndiye Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana. Yeye ni Mungu mkuu na mwenye nguvu, na wa kuogofya; hapendelei wala hapokei rushwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani Bwana Mungu wenu ni Mungu wa miungu, ni Bwana wa mabwana, ni Mungu mkubwa atishaye kwa matendo ya nguvu, hapendelei uso wa mtu, hachukui mapenyezo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana Yawe, Mungu wenu, ndiye Mungu wa miungu na Bwana wa wabwana. Yeye ni Mungu mukubwa na mwenye nguvu, na wa kuogopesha. Hapendelei wala hapokei kituliro.