Deuteronomy 11:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafundisheni watoto wenu maneno haya mkiyazungumzia mketipo katika nyumba zenu, mnapotembea, mnapolala na mnapoamka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wafundisheni watoto wenu, yazungumzeni mnapoketi nyumbani na mnapotembea njiani, mnapolala na mnapoamka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafundisheni watoto wenu maneno haya mkiyazungumzia mketipo katika nyumba zenu, mnapotembea, mnapolala na mnapoamka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wafundisheni watoto wenu, yazungumzeni wakati mketipo nyumbani na wakati mtembeapo njiani, wakati mlalapo na wakati mwamkapo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wafundisheni watoto wenu, yazungumzeni wakati mketipo nyumbani na wakati mtembeapo njiani, wakati mlalapo na wakati mwamkapo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo wafunzeni watoto wenu kwa kuyazungumza uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafundisheni watoto wenu maneno haya mkiyazungumzia mketipo katika nyumba zenu, mnapotembea, mnapolala na mnapoamka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yafundisheni watoto wenu na kuyasema nao ukikaa nyumbani mwako, ukienda safari zako, ukitaka kulala, hata ukiamka!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muwafundishe watoto wenu maneno haya mukiyazungumuzia munapoikaa katika nyumba zenu, munapotembea, munapolala na munapoamuka.