Deuteronomy 11:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mkijihadhari kutenda amri zote ambazo nimewapa: Kumpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuzifuata njia zake zote na kuambatana naye,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkizingatia kwa makini maagizo haya yote ninayowapa kuyafuata, ya kumpenda Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kuenenda katika njia zake zote na kushikamana naye kwa uthabiti,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa kwamba mtayashika kwa bidii maagizo haya yote niwaagizayo, kuyafanya; kumpenda Bwana, Mungu wenu, na kutembea katika njia zake zote, na kushikamana naye;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mkijihadhari kutenda amri zote ambazo nimewapa: kumpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuzifuata njia zake zote na kuambatana naye,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mkishika kwa makini maagizo haya yote ninayowapa kuyafuata, ya kumpenda BWANA Mungu wenu, kuenenda katika njia zake zote na kushikamana naye kwa uthabiti,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mkishika kwa makini maagizo haya yote ninayowapa kuyafuata, ya kumpenda bwana Mwenyezi Mungu wenu, kuenenda katika njia zake zote na kushikamana naye kwa uthabiti,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa kama mtayazingatia kwa bidii maagizo haya yote niwaagizayo, kuyafanya; kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kutembea katika njia zake zote, na kushikamana naye;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mkijihadhari kutenda amri zote ambazo nimewapa: Kumpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuzifuata njia zake zote na kuambatana naye,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mtakapoyaangalia vema haya maagizo yote, mimi ninayowaagiza ninyi, myafanye na kumpeda Bwana Mungu wenu na kuzishika njia zake na kugandamana naye,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa kwamba mtayashika kwa bidii maagizo haya yote niwaagizayo, kuyafanya; kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kutembea katika njia zake zote, na kushikamana naye;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kama mukishika amri zote ambazo nimewapa, mukimupenda Yawe, Mungu wenu, na kufuata njia zake zote na kuambatana naye,