Deuteronomy 11:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hakuna mtu yeyote atakayeweza kuwakabili. Popote mtakapokwenda katika nchi hiyo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawatia watu hofu wawaogope, kama alivyowaahidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama dhidi yenu. Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kama alivyoahidi, ataweka juu ya nchi yote utisho na hofu kwa ajili yenu popote mtaenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama mbele yenu; Bwana, Mungu wenu, ataweka utisho wenu na kuhofiwa kwenu juu ya nchi yote mtakayoikanyaga, kama alivyowaambia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hakuna mtu yeyote atakayeweza kuwakabili. Popote mtakapokwenda katika nchi hiyo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawatia watu hofu wawaogope, kama alivyowaahidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama dhidi yenu. BWANA Mungu wenu, kama alivyoahidi, ataweka juu ya nchi yote utisho na hofu kwa ajili yenu po pote mwendako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama dhidi yenu. bwana Mwenyezi Mungu wenu, kama alivyoahidi, ataweka juu ya nchi yote utisho na hofu kwa ajili yenu popote mwendako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama mbele yenu; BWANA, Mungu wenu, ataweka utisho wenu na kuhofiwa kwenu juu ya nchi yote mtakayoikanyaga, kama alivyowaambia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hakuna mtu yeyote atakayeweza kuwakabili. Popote mtakapokwenda katika nchi hiyo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawatia watu hofu wawaogope, kama alivyowaahidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hatakuwako mtu atakayeweza kusimama mbele yenu, kwani Bwana Mungu wenu atawastusha, wawaogope ninyi katika nchi zote, mtakazozikanyaga, kama alivyowaambia ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama mbele yenu; BWANA, Mungu wenu, ataweka utisho wenu na kuhofiwa kwenu juu ya nchi yote mtakayoikanyaga, kama alivyowaambia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakuna mutu yeyote atakayeweza kuwashambulia. Popote mutakapokwenda katika inchi hiyo, Yawe, Mungu wenu, atawatia watu hofu wawaogope, kama vile alivyowaahidi.