Deuteronomy 11:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu atakapowafikisha kwenye nchi mnayokwenda kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka mlima Gerizimu, na laana kutoka mlima Ebali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atakapokuwa amewaleta katika nchi mnayoiingia kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka Mlima Gerizimu, na kutangaza laana kutoka Mlima Ebali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa, atakapokuleta Bwana, Mungu wako, na kukutia katika nchi uendeayo kuimiliki, ndipo uiweke baraka juu ya mlima wa Gerizimu, na laana uiweke juu ya mlima wa Ebali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu atakapowafikisha kwenye nchi mnayokwenda kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka mlima Gerizimu, na laana kutoka mlima Ebali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati BWANA Mungu wenu atakapokuwa amewaleta katika nchi mnayoiingia kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka Mlima Gerizimu, na kutangaza laana kutoka Mlima Ebali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapokuwa amewaleta katika nchi mnayoiingia kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka Mlima Gerizimu, na kutangaza laana kutoka Mlima Ebali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa, atakapokuleta BWANA, Mungu wako, na kukutia katika nchi uiendeayo kuimiliki, ndipo uiweke baraka juu ya mlima wa Gerizimu, na laana uiweke juu ya mlima wa Ebali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu atakapowafikisha kwenye nchi mnayokwenda kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka mlima Gerizimu, na laana kutoka mlima Ebali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, Bwana Mungu wako atakapokuingiza katika nchi hiyo, wewe utakayoiingia kuichukua, iwe yako, ndipo utoe mbaraka juu ya mlima wa Gerizimu, nacho kiapizo juu ya mlima wa Ebali
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa, atakapokuleta BWANA, Mungu wako, na kukutia katika nchi uendeayo kuimiliki, ndipo uiweke baraka juu ya mlima wa Gerizimu, na laana uiweke juu ya mlima wa Ebali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe atakapowafikisha kwenye inchi munayokwenda kurizi, mutatangaza baraka kutoka kwenye mulima Gerizimu, na laana kutoka kwenye mulima Ebali.