Deuteronomy 12:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mtakapovuka mto Yordani na kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawapa mu irithi, na atakapowapatia pumziko msisumbuliwe na adui zenu wote watakaowazunguka ili muishi salama,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mtakapovuka Yordani na kukaa katika nchi anayowarithisha Bwana, Mungu wenu, akawapeni raha, akiwaokoa na adui zenu pande zote, mkakaa salama;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mtakapovuka mto Yordani na kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawapa muirithi, na atakapowapatia pumziko msisumbuliwe na adui zenu wote watakaowazunguka ili muishi salama,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchi BWANA Mungu wenu anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchi bwana Mwenyezi Mungu wenu anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mtakapovuka Yordani na kukaa katika nchi anayowarithisha BWANA, Mungu wenu, akawapeni raha, akiwaokoa na adui zenu pande zote, mkakaa salama;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mtakapovuka mto Yordani na kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawapa mu irithi, na atakapowapatia pumziko msisumbuliwe na adui zenu wote watakaowazunguka ili muishi salama,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mtauvuka Yordani, mpate kukaa katika nchi hiyo, Bwana Mungu wenu atakayowapa, iwe fungu lenu; ndiko, atakakowapatia kupumzika kwa kuwashinda adui zenu wote pande zote, mkae na kutulia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mtakapovuka Yordani na kukaa katika nchi anayowarithisha BWANA, Mungu wenu, akawapeni raha, akiwaokoa na adui zenu pande zote, mkakaa salama;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mutakapovuka muto Yordani na kuishi katika inchi ambayo Yawe, Mungu wenu, atawapatia muirizi, na atakapowapatia pumziko musisumbuliwe na waadui zenu wote watakaowazunguka kusudi mupate kuishi salama,