Deuteronomy 12:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
basi huko mahali Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atakapochagua ili jina lake likae, hapo ndipo mtakapopeleka kila kitu ninachowaamuru: Tambiko zenu za kuteketeza na sadaka zenu, zaka zenu na matoleo yenu, na sadaka zenu za nadhiri mnazoahidi kumtolea Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha kuhusu mahali Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atakapopachagua kuwa makao ya Jina lake, hapo ndipo inapowapasa kuleta kila kitu ninachowaamuru: sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo, pamoja na vitu vyote vyenye thamani ambavyo mmeweka nadhiri kumtolea Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua Bwana, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
basi huko mahali Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atakapochagua ili jina lake likae, hapo ndipo mtakapopeleka kila kitu ninachowaamuru: tambiko zenu za kuteketeza na sadaka zenu, zaka zenu na matoleo yenu, na sadaka zenu za nadhiri mnazoahidi kumtolea Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha kuhusu mahali BWANA Mungu wenu atakapopachagua kuwa mahali pa makao ya Jina lake, hapo ndipo inapowapasa kuleta kila kitu ninachowaamuru: sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo, pamoja na vitu vyote vyenye thamani ambavyo mmeweka nadhiri kumtolea BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha kuhusu mahali bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapopachagua kuwa mahali pa makao ya Jina lake, hapo ndipo inapowapasa kuleta kila kitu ninachowaamuru: sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo, pamoja na vitu vyote vyenye thamani ambavyo mmeweka nadhiri kumtolea bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
basi huko mahali Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atakapochagua ili jina lake likae, hapo ndipo mtakapopeleka kila kitu ninachowaamuru: Tambiko zenu za kuteketeza na sadaka zenu, zaka zenu na matoleo yenu, na sadaka zenu za nadhiri mnazoahidi kumtolea Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mahali pale, Bwana Mungu wenu atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake, sharti mpeleke hapo yote, mimi ninayowaagiza leo: ng'ombe zenu za tambiko za uteketezwa nzima na ng'ombe zenu nyingine za tambiko na mafungu yenu ya kumi na vipaji vya mikono yenu vya tambiko vya kunyanyuliwa, nayo yote ya kuyalipa, mliyoyaapa kumtolea Bwana kwa kupenda wenyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
basi huko pahali Yawe, Mungu wenu, atakapochagua kusudi jina lake likae pale, hapo mutapeleka yote ninayowaamuru: sadaka zenu za kuteketeza kwa moto na sadaka zingine, sehemu ya kumi za mazao yenu, na sadaka za kutimiza kiapo.