Deuteronomy 12:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini mna uhuru wa kuchinja na kula wanyama wenu popote katika makao yenu mnavyopenda, kama baraka za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alizowapa, kadiri mtakavyojaliwa na Mwenyezi-Mungu. Watu wote, walio safi au najisi wanaweza kula nyama hizo, kama vile mlavyo nyama ya paa au ya kulungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, mnaweza kuwachinja wanyama wenu katika miji yenu yoyote ile na kula nyama nyingi mpendavyo kama vile mmemchinja paa au kulungu, kulingana na baraka mtakazojaliwa na Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Watu walio najisi na walio safi wanaweza kula.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pamoja na haya waweza kuchinja nyama na kula ndani ya malango yako yote, kwa kufuata yote yatamaniwayo na roho yako, kwa mfano wa baraka ya Bwana, Mungu wako, aliyokupa; aliye tohara na asiye tohara ana ruhusa kula katika nyama hiyo, kama ya paa na ya kulungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini mna uhuru wa kuchinja na kula wanyama wenu popote katika makao yenu mnavyopenda, kama baraka za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alizowapa, kadiri mtakavyojaliwa na Mwenyezi-Mungu. Watu wote, walio safi au najisi wanaweza kula nyama hizo, kama vile mlavyo nyama ya paa au ya kulungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, mnaweza kuwachinja wanyama wenu katika miji yenu yo yote ile na kula nyama nyingi mpendavyo kama vile mmemchinja paa au kulungu, kulingana na baraka mtakazojaliwa na BWANA Mungu wenu. Watu walio najisi au walio safi wanaweza kula.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, mnaweza kuwachinja wanyama wenu katika miji yenu yoyote ile na kula nyama nyingi mpendavyo kama vile mmemchinja paa au kulungu, kulingana na baraka mtakazojaliwa na bwana Mwenyezi Mungu wenu. Watu walio najisi au walio safi wanaweza kula.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pamoja na haya, waweza kuchinja nyama na kula ndani ya malango yako yote, kwa kufuata yote yanayotamaniwa na roho yako, kulingana na baraka ya BWANA, Mungu wako, aliyokupa; aliye tohara na asiye tohara ana ruhusa kula katika nyama hiyo, kama ya paa na ya kulungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini mna uhuru wa kuchinja na kula wanyama wenu popote katika makao yenu mnavyopenda, kama baraka za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alizowapa, kadiri mtakavyojaliwa na Mwenyezi-Mungu. Watu wote, walio safi au najisi wanaweza kula nyama hizo, kama vile mlavyo nyama ya paa au ya kulungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini roho yako ikiwa na uchu wa nyama tu, utazichinja na kuzila malangoni pako po pote kwa mbaraka ya Bwana Mungu wako aliyekupa hizo nyama; mwenye uchafu na mwenye kutakata atazila, kama ni za paa au kama ni za kulungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pamoja na haya waweza kuchinja nyama na kula ndani ya malango yako yote, kwa kufuata yote yatamaniwayo na roho yako, kwa mfano wa baraka ya BWANA, Mungu wako, aliyokupa; aliye tohara na asiye tohara ana ruhusa kula katika nyama hiyo, kama ya paa na ya kulungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Lakini muna uhuru wa kuchinja na kula nyama wenu popote katika makao yenu munavyopenda, kama vile baraka za Yawe, Mungu wenu, alizowapa, kadiri mutakavyojaliwa na Yawe. Watu wote, wanaokuwa safi au wachafu wanaweza kula, kama vile munavyokula nyama ya paa au ya kulungu.