Deuteronomy 12:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msile vitu vifuatavyo mahali mnapoishi: Zaka ya nafaka zenu, wala ya divai yenu, wala ya mafuta yenu, wala ya wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe au kondoo wenu, wala sadaka zenu za nadhiri au tambiko zenu za hiari, wala matoleo mengineyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hamruhusiwi kula katika miji yenu zaka yenu ya nafaka, ya divai mpya na ya mafuta, au mzaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na makundi yenu ya mbuzi na kondoo, wala chochote ambacho mmeweka nadhiri kukitoa, au sadaka zako za hiari, wala matoleo maalum.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Usile ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng'ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zo zote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msile vitu vifuatavyo mahali mnapoishi: zaka ya nafaka zenu, wala ya divai yenu, wala ya mafuta yenu, wala ya wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe au kondoo wenu, wala sadaka zenu za nadhiri au tambiko zenu za hiari, wala matoleo mengineyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hamruhusiwi kula katika miji yenu zaka yenu ya nafaka, ya divai mpya na ya mafuta, au mzaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng'ombe na makundi yenu ya mbuzi na kondoo, wala cho chote ambacho mmeweka nadhiri kukitoa, au sadaka zako za hiari, wala matoleo maalum.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hamruhusiwi kula katika miji yenu zaka yenu ya nafaka, ya divai mpya na ya mafuta, au mzaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na makundi yenu ya mbuzi na kondoo, wala chochote ambacho mmeweka nadhiri kukitoa, au sadaka zako za hiari, wala matoleo maalum.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Usile ndani ya makazi yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng'ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zozote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msile vitu vifuatavyo mahali mnapoishi: Zaka ya nafaka zenu, wala ya divai yenu, wala ya mafuta yenu, wala ya wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe au kondoo wenu, wala sadaka zenu za nadhiri au tambiko zenu za hiari, wala matoleo mengineyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ni mwiko kula malangoni pako fungu la kumi la ngano zako, nalo la mvinyo zako mbichi, nalo la mafuta yako, nao wana wa kwanza wa ng'ombe wako nao wana wa kwanza wa mbuzi wako na wa kondoo wako, nayo yo yote ya kuyalipa uliyoyaapa, nayo matoleo yako, utakayoyatoa kwa kupenda mwenyewe, navyo vipaji vya mikono yako vya tambiko vya kunyanyuliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Usile ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng’ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zo zote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikule vitu hivi pahali munapoishi: sehemu ya kumi za ngano zenu, divai zenu au mafuta yenu, wazaliwa wa kwanza wa ngombe wenu au kondoo wenu, au sadaka zenu za kutimiza kiapo au za mapenzi, au matoleo mengine.