Deuteronomy 12:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtavila vitu hivyo mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mahali atakapopachagua Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Mtavila nyinyi pamoja na watoto wenu wa kiume na wa kike, watumishi wenu wa kiume na wa kike, na Walawi wanaoishi katika miji yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Badala yake, mtakula vitu hivyo katika uwepo wa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, mahali Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atakapopachagua: wewe, wana wako na binti zako, watumishi wako wa kiume na wa kike, na Walawi kutoka miji yenu. Mnatakiwa mfurahi mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa kula kitu mtakachoweka mikono yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini hivyo mtakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, wewe, na mwanao mume na mke, na mtumwa wako mume na mke, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za Bwana, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtavila vitu hivyo mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mahali atakapopachagua Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Mtavila nyinyi pamoja na watoto wenu wa kiume na wa kike, watumishi wenu wa kiume na wa kike, na Walawi wanaoishi katika miji yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Badala yake, mtakula vitu hivyo katika uwepo wa BWANA Mungu wenu mahali ambapo BWANA Mungu wenu atapachagua: wewe, wana wako na binti zako, watumishi wako wa kiume na wa kike, na Walawi kutoka miji yenu. Mnatakiwa mfurahi mbele za BWANA Mungu wenu kwa kula kitu mtakachoweka mikono yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Badala yake, mtakula vitu hivyo katika uwepo wa bwana Mwenyezi Mungu wenu mahali ambapo bwana Mwenyezi Mungu wenu atapachagua: wewe, wana wako na binti zako, watumishi wako wa kiume na wa kike, na Walawi kutoka miji yenu. Mnatakiwa mfurahi mbele za bwana Mwenyezi Mungu wenu kwa kula kitu mtakachoweka mikono yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini hivyo mtakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, wewe, na mwanao wa kiume na wa kike, na mtumwa wako wa kiume na wa kike, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtavila vitu hivyo mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mahali atakapopachagua Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Mtavila nyinyi pamoja na watoto wenu wa kiume na wa kike, watumishi wenu wa kiume na wa kike, na Walawi wanaoishi katika miji yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya yote utayala mbele ya Bwana Mungu wako mahali pale tu, Bwana Mungu wako atakapopachagua; hapo na uyale wewe na wana wako wa kiume na wa kike na watumishi wako wa kiume na wa kike, naye Mlawi aliopo malangoni pako, upate kuyafurahia mbele ya Bwana yote, mikono yako iliyoyachukua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini hivyo mtakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, wewe, na mwanao mume na mke, na mtumwa wako mume na mke, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutavikula mbele ya Yawe, Mungu wenu, pahali Yawe, Mungu wenu, atakapochagua. Mutavikula ninyi pamoja na wana wenu na wabinti zenu, watumishi wenu na wajakazi wenu, na Walawi wanaoishi katika miji yenu.