Deuteronomy 12:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atakapoipanua nchi yenu, kama alivyoahidi, nanyi mtasema, ‘Tutakula nyama’, kwa vile mnapenda kula nyama, mnaweza kula nyama kiasi chochote mnachotaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atakapokuwa ameongeza nchi yenu kama alivyowaahidi, nanyi mkitamani nyama na mkisema, “Ningependa nyama,” hapo unaweza kula nyingi upendavyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana, Mungu wako, atakapoongeza mpaka wako, kama alivyokuahidi, nawe utakaposema, Nataka kula nyama, kwa kuwa roho yako yatamani kula nyama; waweza kula nyama, kwa kufuata yote inayotamani roho yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atakapoipanua nchi yenu, kama alivyoahidi, nanyi mtasema, ‘Tutakula nyama’, kwa vile mnapenda kula nyama, mnaweza kula nyama kiasi chochote mnachotaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mungu wenu atakapokuwa ameongeza nchi yenu kama alivyowaahidi, nanyi mkitamani nyama na mkisema, “Ningependa nyama,” hapo unaweza kula nyingi upendavyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapokuwa ameongeza nchi yenu kama alivyowaahidi, nanyi mkitamani nyama na mkisema, “Ningependa nyama,” hapo unaweza kula nyingi upendavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA, Mungu wako, atakapoongeza mpaka wako, kama alivyokuahidi, nawe utakaposema, Nataka kula nyama, kwa kuwa roho yako yatamani kula nyama; waweza kula nyama, kwa kufuata yote inayotamani roho yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atakapoipanua nchi yenu, kama alivyoahidi, nanyi mtasema, ‘Tutakula nyama’, kwa vile mnapenda kula nyama, mnaweza kula nyama kiasi chochote mnachotaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mungu wako atakapoipanua mipaka yako, kama alivyokuambia, nawe utakaposema: Nataka kula nyama, kwani roho yangu ina uchu wa nyama, basi, na ule nyama kwa huo uchu wote wa roho yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA, Mungu wako, atakapoongeza mpaka wako, kama alivyokuahidi, nawe utakaposema, Nataka kula nyama, kwa kuwa roho yako yatamani kula nyama; waweza kula nyama, kwa kufuata yote inayotamani roho yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Yawe, Mungu wenu atakapopanua inchi yenu, kama vile alivyoahidi, nanyi mutasema: ‘Tutakula nyama’ kwa sababu munapenda nyama, munaweza kula nyama kiasi munachotaka.