Deuteronomy 12:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mahali atakapochagua Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aweke jina lake, hapo mnaweza kuchinja ng'ombe au kondoo yeyote ambaye Mwenyezi-Mungu amewajalia, kama nilivyowaamuru, na mnaweza kula kiasi chochote mnachotaka cha nyama hiyo, kama mkiwa katika miji yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mahali Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atakapopachagua kuweka Jina lake ni mbali sana kutoka kwenu, unaweza kuchinja wanyama kutoka makundi yenu ya ng’ombe, ya mbuzi na ya kondoo ambayo Mwenyezi Mungu amewapa, kama nilivyokuamuru, na mkiwa katika miji yenu wenyewe mnaweza kula nyingi mtakavyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, apaweke jina lake, pakiwa mbali nawe mno, ndipo utakapochinja katika kundi lako la ng'ombe na kondoo alilokupa Bwana kama nilivyokuagiza, nawe utakula ndani ya malango yako, kwa kufuata yote inayotamani roho yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mahali atakapochagua Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aweke jina lake, hapo mnaweza kuchinja ng'ombe au kondoo yeyote ambaye Mwenyezi-Mungu amewajalia, kama nilivyowaamuru, na mnaweza kula kiasi chochote mnachotaka cha nyama hiyo, kama mkiwa katika miji yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mahali ambapo BWANA Mungu wenu atapachagua kuweka Jina lake ni mbali sana kutoka kwenu, unaweza kuchinja wanyama kutoka makundi yenu ya ng'ombe, ya mbuzi na ya kondoo ambayo BWANA amewapa, kama nilivyokuamuru, na mkiwa katika miji yenu wenyewe mnaweza kula nyingi mtakavyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mahali ambapo bwana Mwenyezi Mungu wenu atapachagua kuweka Jina lake ni mbali sana kutoka kwenu, unaweza kuchinja wanyama kutoka makundi yenu ya ng’ombe, ya mbuzi na ya kondoo ambayo bwana amewapa, kama nilivyokuamuru, na mkiwa katika miji yenu wenyewe mnaweza kula nyingi mtakavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apaweke jina lake, pakiwa mbali nawe mno, ndipo utakapochinja katika kundi lako la ng'ombe na kondoo alilokupa BWANA kama nilivyokuagiza, nawe utakula ndani ya malango yako, kwa kufuata yote inayotamani roho yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mahali atakapochagua Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aweke jina lake, hapo mnaweza kuchinja ng'ombe au kondoo yeyote ambaye Mwenyezi-Mungu amewajalia, kama nilivyowaamuru, na mnaweza kula kiasi chochote mnachotaka cha nyama hiyo, kama mkiwa katika miji yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama mahali pale, Bwana Mungu atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake, patakuwa mbali kutoka kwako, basi, na utoe wa kuchinja katika ng'ombe wako au katika mbuzi na kondoo wako, Bwana aliokupa, ule nyama, kama nilivyokuagiza, malangoni pako, uukomeshe uchu wote wa roho yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apaweke jina lake, pakiwa mbali nawe mno, ndipo utakapochinja katika kundi lako la ng’ombe na kondoo alilokupa BWANA kama nilivyokuagiza, nawe utakula ndani ya malango yako, kwa kufuata yote inayotamani roho yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, pahali Yawe, Mungu wenu, atakapochagua, apaweke jina lake, hapo munaweza kuchinja ngombe au kondoo yeyote ambaye Yawe amewajalia, kama nilivyowaamuru na munaweza kula kiasi chochote munachotaka cha nyama hiyo, kama mukiwa katika miji yenu.