Deuteronomy 12:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msimwabudu hivyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa maana kila chukizo ambalo Mwenyezi-Mungu hapendi, wameifanyia miungu yao; hata wamewachoma motoni watoto wao wa kiume na wa kike, ili kuitambikia miungu yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kamwe msimwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa njia wanayoabudu miungu yao, kwa sababu katika kuabudu miungu yao, wanafanya aina zote za machukizo anayoyachukia Mwenyezi Mungu. Hata huwateketeza watoto wao wa kiume na wa kike motoni kama kafara kwa miungu yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Usimtende kama haya Bwana, Mungu wako; kwani kila yaliyo machukizo kwa Bwana, ayachukiayo yeye, wameifanyia miungu yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msimwabudu hivyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa maana kila chukizo ambalo Mwenyezi-Mungu hapendi, wameifanyia miungu yao; hata wamewachoma motoni watoto wao wa kiume na wa kike, ili kuitambikia miungu yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kamwe msimwabudu BWANA Mungu wenu kwa njia wanayoabudu miungu yao, kwa sababu katika kuabudu miungu yao, wanafanya aina zote za machukizo anayoyachukia BWANA. Hata huwateketeza wana wao na binti zao kwa moto kama kafara kwa miungu yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kamwe msimwabudu bwana Mwenyezi Mungu wenu kwa njia wanayoabudu miungu yao, kwa sababu katika kuabudu miungu yao, wanafanya aina zote za machukizo anayoyachukia bwana. Hata huwateketeza wana wao na binti zao kwa moto kama kafara kwa miungu yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Usimtende kama haya BWANA, Mungu wako; kwani kila yaliyo machukizo kwa BWANA, ayachukiayo yeye, wameifanyia miungu yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msimwabudu hivyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa maana kila chukizo ambalo Mwenyezi-Mungu hapendi, wameifanyia miungu yao; hata wamewachoma motoni watoto wao wa kiume na wa kike, ili kuitambikia miungu yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Usimfanyizie Bwana Mungu wako hivyo! Kwani yote yaliyo matapisho kwake Bwana kwa kuyachukia waliifanyizia miungu yao, kwani nao wana wao wa kiume na wa kike waliitolea miungu yao na kuwateketeza motoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Usimtende kama haya BWANA, Mungu wako; kwani kila yaliyo machukizo kwa BWANA, ayachukiayo yeye, wameifanyia miungu yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musimwabudu Yawe, Mungu wenu, hivyo, kwa maana kila chukizo ambalo Yawe hapendi, wameifanyia miungu yao, hata wamewachoma ndani ya moto watoto wao wanaume na wanawake, kwa kutambikia miungu yao.